1 Timothy 6

1Wale wote walio chini ya nira kama watumwa wawachukulie mabwana zao kama wenye heshima zote, wanatakiwa kufanya hivyo ili jina la Mungu na mafundisho yasitukanwe. 2Watumwa wenye mabwana waaminio wasiwadharau kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie zaidi. Kwa sababu mabwana wanaosaidiwa kazi zao ni waamini na wanapendwa. Fundisha na kuyatangaza mambo haya.

3Iwapo mtu fulani anafundisha kwa upotovu na hayapokei maelekezo yetu yenye kuaminika, ambayo ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo, iwapo hawalikubali fundisho liongozalo kwenye utauwa. 4Mtu huyo anajivuna na hajui chochote. Badala yake, ana vurugu na mabishano juu ya maneno. Maneno haya huzaa wivu, ugomvi, matukano, shuku mbaya, 5na vurugu za mara kwa mara kati ya watu wenye akili zilizoharibika. Wanaiacha kweli. Wanafikiri kwamba utauwa ni njia ya kuwa matajiriā€

6Sasa utauwa na kuridhika ni faida kubwa. 7Kwa maana hatukuja na chochote duniani. Wala hatuwezi kuchukua chochote kutoka duniani. 8Badala yake, tutosheke na chakula na mavazi.

9Sasa hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego. Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya, na katika kitu chochote kinachowafanya watu wazame katika maangamizi na uharibifu. 10Kwa kuwa kupenda fedha ni chanzo cha aina zote za uovu. Watu ambao hutamani hiyo, wamepotoshwa mbali na imani na wamejichoma wenyewe kwa huzuni nyingi.

11Lakini wewe mtu wa Mungu, yakimbie mambo hayo. Fuata haki, utauwa, uaminifu, upendo, usitahimilivu, na upole. 12Piga vita vizuri vya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba ulitoa ushuhuda mbele ya mashahidi wengi kwa kile kilicho chema.

13Nakupa amri hii mbele za Mungu, anayesababisha vitu vyote kuishi, na mbele ya Yesu Kristo, aliyenena iliyo kweli kwa Pontio Pilato: 14itunze amri kwa ukamilifu, pasipo mashaka, hadi ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo.

15Mungu atadhihirisha ujio wake kwa wakati sahihi- Mungu, Mbarikiwa, nguvu pekee, Mfalme anayetawala, Bwana anayeongoza. 16Peke yake anaishi milele na akaaye katika mwanga usiokaribiriwa. Hakuna mtu awezaye kumwona wala awezaye kumtazama. Kwake iwe heshima na uweza wa milele. Amina.

17Waambie matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, na wasitumaini katika utajiri, ambao siyo wa uhakika. Badala yake, wanapaswa kumtumaini Mungu. Ambaye hutupatia utajiri wote wa kweli ili tufurahie. 18Waambie watende mema, watajirike katika kazi njema, wawe wakarimu, na utayari wa kutoa. 19Katika njia hiyo watajiwekea msingi mzuri kwa mambo yajayo, ili kwamba waweze kushika maisha halisi.

20Timotheo, linda kile ulichopewa. Jiepushe na majadiliano ya kipumbavu na mabishano yenye kujipinga ambayo kwa kwa uongo huitwamaarifa. 21Baadhi ya watu huyatangaza mambo haya, na hivyo wameikosa imani. Neema na iwe pamoja nawe.

Copyright information for SwaULB